Walioitwa Kwenye Usaili Muhimbili (MNH) 2025

Walioitwa Kwenye Usaili Muhimbili (MNH) 2025

  • Posted by:
  • Posted on:
  • Category:
    AjiraAjira
  • System:
    Unknown
  • Price:
    USD 0

Katika makala360 leo, Hii hapa orodha ya majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Muhimbili (MNH) 2025 Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 06-05-2025 hadi 07-05-2025 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

Kuitwa kwenye Usaili Muhimbili

Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.

Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)

Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;

Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka.

Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.

Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.

Usaili Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.

Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.

Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)

Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.

Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.

Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili.

Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.

Pakua PDF hapa.

Soma zaidi:

  1. Walioitwa Kwenye Usaili NECTA 2025
  2. Walioitwa Kazini TAWA 2025
  3. Walioitwa Kazini TFS 2025
  4. Walioitwa Kazini Benki Kuu ya Tanzania (BOT)
Tagged:
,
Rating

0

( 0 Votes )
Please Rate!
Walioitwa Kwenye Usaili Muhimbili (MNH) 2025

No votes so far! Be the first to rate this post.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *