NECTA Matokeo ya Kidato cha Pili 2023-24

NECTA Matokeo ya Kidato cha Pili 2023-24

  • Posted by:
  • Posted on:
  • Category:
    ElimuElimu
  • System:
    Unknown
  • Price:
    USD 0

Leo katika makala360, Haya hapa Matokeo ya Kidato cha pili 2023-24 NECTA Katika Mkutano wake wa 157 uliofanyika tarehe 07 Januari, 2023 katika ofisi za Baraza la Mitihani la Tanzania zilizopo Dar es Salaam, Baraza la Mitihani la Tanzania liliidhinisha kutangazwa rasmi kwa matokeo ya Kidato cha Pili iliyofanyika mwezi Oktoba/Novemba, 2023.

Jumla ya wanafunzi 759,799 walisajiliwa kufanya Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili wakiwemo Wasichana 405,878 sawa na asilimia 53.42 na Wavulana 353,921 sawa na asilimia 46.58. Kati ya wanafunzi waliosajiliwa, wanafunzi 695,639 walifanya Upimaji, wakiwemo Wasichana 376,927 (92.87%) na Wavulana 318,712 (90.05%). Wanafunzi 64,160 (8.44%) hawakufanya Upimaji, kati yao Wasichana ni 28,951 (7.13%) na Wavulana ni 35,209 (9.95%).

Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili

Jumla ya wanafunzi 592,741 kati ya 694,769 wenye matokeo ambao ni sawa na asilimia 85.31 wamefaulu ambapo wamepata Madaraja 5 ya I, II, III na IV. Mwaka 2022 Wanafunzi waliofaulu walikuwa 539,645 sawa na asilimia 85.18.

Hivyo, kumekuwa na ongezeko la ufaulu kwa asilimia 0.13 pamoja na ongezeko la idadi ya wanafunzi 53,096 sawa na asilimia 9.84 ya wanafunzi waliopata fursa ya kuendelea na Kidato cha Tatu ikilinganishwa na mwaka 2022.

Ufaulu wa Shule katika Makundi ya Umahiri

Idadi ya shule katika makundi ya Umahiri inaonesha kuwa, kati ya shule zote 5,515 zenye matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili 2023, shule 5,485 (99.45%) zimepata wastani wa Daraja la A-D ikilinganishwa na shule 5,187 (98.83%) zilizopata wastani wa madaraja hayo mwaka 2022.

Hivyo, kumekuwa na ongezeko la asilimia 0.62 la shule zilizopata wastani wa Daraja la A-D 6 ikilinganishwa na mwaka 2022.

Angalia matokeo hapa.

Soma zaidi:

  1. NECTA Matokeo ya Darasa la Nne 2023
Rating

0

( 0 Votes )
Please Rate!
NECTA Matokeo ya Kidato cha Pili 2023-24

No votes so far! Be the first to rate this post.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *