- Posted by:
- Posted on:
- Category:
ElimuElimu - System:
Unknown - Price:
USD 0
Leo katika makala360 jifunze hili, Baraza la Mitihani la Tanzania hushughulikia maombi ya marekebisho ya majina ya watahiniwa yaliyokosewa katika mitihani ya Shule za Msingi, Sekondari, na Vyuo vya Ualimu. Ifuatayo ni mwongozo rasmi wa jinsi ya kuwasilisha maombi na kufanya marekebisho hayo.
Masharti ya Marekebisho ya Majina
Maombi ya marekebisho yawasilishwe ndani ya mwaka mmoja tangu matokeo ya mtihani yatangazwe.
Jina linalotakiwa kufanyiwa marekebisho ni lazima litofautiane na jina lililotumika katika mtihani wa sifa iliyomuwezesha mtahiniwa kusajiliwa. Lengo ni kufanya jina lifanane na lile lililotumika kwenye mtihani wa sifa.
Marekebisho ya kuongeza, kuondoa, au kubadilisha jina hayaruhusiwi.
Msingi pekee wa kufanya marekebisho ni jina lililoandikwa katika mtihani wa sifa – si jina lililopo kwenye kiapo, cheti cha kuzaliwa, ndoa, ubatizo n.k.
Hatua za Kufuata Wakati wa Kufanya Maombi
Kwa shule: Mkuu wa shule au Mwalimu Mkuu ajaze fomu ya marekebisho au Query Circular Form inayoonyesha kosa lililopo na jina sahihi.
Kwa mzazi au mtahiniwa binafsi: Ajaze fomu ya marekebisho ya jina inayopatikana kwenye tovuti ya NECTA.
Lipia ada ya TZS 35,000 kwa kila cheti kupitia benki za NMB, CRDB, NBC au kwa mitandao ya simu (M-Pesa/Tigo Pesa), kwa kutumia control number kutoka NECTA.
Wasilisha fomu ya maombi kwa NECTA ukiambatanisha:
- Cheti au hati ya matokeo yenye kosa
- Stakabadhi ya malipo
Majibu kwa Mteja
Baada ya marekebisho kufanyika, Hati ya Matokeo au cheti kipya chenye jina sahihi kitatumwa kwa Mkuu wa shule au kwa mtahiniwa binafsi.
Mtahiniwa asiyekuwa na sifa ya kufanyiwa marekebisho atajulishwa kwa barua kuwa marekebisho hayakufanyika.
Soma zaidi: