- Posted by:
- Posted on:
- Category:
AjiraAjira - System:
Unknown - Price:
USD 0
Leo katika makala360, Hii hapa orodha ya majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Chuo Kikuu cha UDSM 2025 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe Mei 15, 2025 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
Usaili utafanyika kuanzia tarehe zilizotajwa kwenye tangazo, na kila msailiwa anatakiwa kufika katika muda na sehemu iliyoainishwa kwa kada yake. Msailiwa anatakiwa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi kama vile Kitambulisho cha Mkazi, cha Mpiga Kura, cha Kazi, cha Uraia au Hati ya Kusafiria. Pia, kila msailiwa anatakiwa kubeba vyeti halisi vya taaluma kuanzia cheti cha kuzaliwa hadi shahada, kutegemeana na sifa za kazi aliyoomba.
Vyeti visivyokubalika ni pamoja na Testimonials, Statement of Results, Provisional Results, na matokeo ya kidato cha IV na VI yasiyo rasmi (results slips); vyeti hivyo havitakubaliwa na wahusika hawataruhusiwa kuendelea na usaili. Wasailiwa wanapaswa kujigharamia chakula, usafiri na malazi, na kuhakikisha wanazingatia tarehe, muda na mahali walipopangiwa usaili. Kwa walio soma nje ya Tanzania, vyeti vyao viwe vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika kama TCU, NACTE au NECTA.
Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana kwenye tangazo wanashauriwa kutokata tamaa, bali waendelee kuomba kazi watakapopata fursa nyingine na kuzingatia vigezo vya tangazo husika. Kwa kada zinazotakiwa kusajiliwa na bodi za kitaaluma, wahusika wanapaswa kuja na vyeti halisi vya usajili na leseni zao. Mwisho, kila msailiwa anatakiwa kuingia kwenye akaunti yake mtandaoni ili kunakili namba ya mtihani, kwani namba hiyo haitatolewa siku ya usaili.
Soma zaidi: