Jinsi ya kusajili Majina ya Biashara BRELA 2025

Jinsi ya kusajili Majina ya Biashara BRELA 2025

  • Posted by:
  • Posted on:
  • Category:
    DodosoDodoso
  • System:
    Unknown
  • Price:
    USD 0

Leo katika makala360, Jifunze Jinsi ya kusajili Majina ya Biashara BRELA 2025 Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ilianzishwa chini ya Sheria ya Wakala za Serikali Na. 30 ya Mwaka 1997 na kuzinduliwa rasmi tarehe 3 Desemba 1999 chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

Jina la biashara ni nini?

Jina la biashara ni utambulisho wa biashara fulani inayofanywa na mtu au kikundi cha watu. Hivyo mtu mmoja au kikundi cha watu wasiozidi 20 wanaweza kusajili jina la biashara. Mfano wa majina ya biashara ni Ali Entreprises, Rose Beauty Salon au John Urassa Investments, n.k

Faida za Urasimishaji wa Jina la Biashara ni zipi?

  1. Kulipa jina la biashara utambulisho wa kisheria
  2. Kulinda jina la biashara lisitumiwe na mtu mwingine.
  3. Kutambulika na taasisi za fedha mf. benki (wakati wa kufungua akaunti).
  4. Kupata mikopo katika taasisi za fedha kama benki.
  5. Kuifanya biashara yako kutambulika kisheria.
  6. Kuitangaza biashara kwa urahisi na kupanua wigo wa wateja.

Vigezo vya kusajili Jina la biashara

  1. Jina la biashara linalokubalika kisheria.
  2. Mwombaji awe Mtanzania.
  3. Awe na umri kuanzia miaka 18.
  4. Namba ya kitambulisho cha taifa (NIN)
  5. Namba ya simu iliyosajiliwa ya kwake binafsi.
  6. Anuani ya baruapepe hai (binafsi)
  7. Anuani ya eneo la biashara.
  8. Anuani ya makazi ya mmiliki au wamiliki wa biashara.

Hatua 10 za kusajili Jina la Biashara

kusajili Jina la Biashara
  1. Tembelea www.brela.go.tz au ors.brela.go.tz
  2. Ingia katika akaunti yako ya Usajili kwa Njia ya Mtandao (ORS) au tengeneza akaunti katika mfumo.
  3. Chagua huduma mtandao
  4. Chagua jina la biashara
  5. Chagua aina ya huduma
  6. Chagua aina ya jina biashara
  7. Jaza taarifa za biashara husika
  8. Pakia viambatisho katika mfumo.
  9. Fanya malipo kwa njia ya simu au benki.
  10. Maombi yatafanyiwa kazi baada ya malipo kupokewa.

Soma makala zaidi:

  1. Jinsi ya Kusajili Kampuni BRELA 2025
  2. Nafasi za Kazi Qatar Airways Tanzania 2025
  3. Matokeo ya Usaili Air Tanzania (ATCL) 2025
  4. Nafasi za Kazi Mwanga Hakika Bank Tanzania 2025
  5. Nafasi za Kazi Strategis Insurance Tanzania 2025
Tagged:
Rating

0

( 0 Votes )
Please Rate!
Jinsi ya kusajili Majina ya Biashara BRELA 2025

No votes so far! Be the first to rate this post.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *