- Posted by:
- Posted on:
- Category:
AjiraAjira - System:
Unknown - Price:
USD 0
Leo katika makala 360, Jinsi ya Kutuma Malalamiko Matokeo ya Usaili TRA 2025 Angalia hapa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuwataarifu waombaji wote waliofanya usaili wa mchujo wa kuandika kuwa, kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya usaili huo mnamo tarehe 26 Aprili, 2025, fursa imetolewa kwa wale wote wenye malalamiko au wanaohitaji ufafanuzi kuhusu matokeo hayo.
Kwa kuzingatia umuhimu wa haki na uwazi katika mchakato wa ajira, wasailiwa wana malalamiko au hoja zozote wanahimizwa kuwasilisha barua rasmi ya malalamiko kwa Kamishna Mkuu wa TRA kuanzia tarehe 28 hadi 29 Aprili, 2025. Barua hiyo inapaswa kueleza kwa kina sababu za malalamiko na kuambatanishwa na namba ya mtihani ya msailiwa husika.
Njia za kuwasilisha malalamiko ni kama ifuatavyo:
- Kwa njia ya barua pepe:
Tuma kupitia anwani zifuatazo:
huduma@tra.go.tz au services@tra.go.tz - Kwa waliopo Dar es Salaam:
Wanaweza kufikisha barua moja kwa moja kwenye Ofisi ya TRA, Kituo cha Huduma kwa Mlipa Kodi kilichopo Mtaa wa Samora, katika saa za kazi.
TRA inasisitiza kuwa barua zitakazowasilishwa nje ya muda uliopangwa hazitashughulikiwa. Hii ni fursa ya kipekee ya kuhakikisha kuwa haki inatendeka kwa kila msailiwa.
Soma makala zaidi: