NACTVET Yazindua Kampeni ya “Mwanachuo Smart” kwa Ajili ya Kukuza Uelewa wa Kidijitali Miongoni mwa Wanafunzi
[siteseo_toc]
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limezindua rasmi kampeni mpya inayojulikana kama “Mwanachuo Smart”, yenye lengo la kukuza uelewa wa wanafunzi wa ngazi ya Astashahada na Stashahada kuhusu matumizi ya mifumo mbalimbali ya kidijitali ya NACTVET.
[dlpro-gallery image_url=”https://makala360.com/wp-content/uploads/2025/05/Mwanachuo-Smart-NACTVET.png”%5D
Kampeni hiyo ilizinduliwa tarehe 6 Mei 2025 na Katibu Mtendaji wa NACTVET, Dkt. Mwajuma Lingwanda, ambapo hafla hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi kutoka TAHLISO pamoja na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini.
Mifumo Itakayotumika na Wanafunzi
Kupitia kampeni hii, NACTVET inawahamasisha wanafunzi kutumia mifumo ifuatayo, inayopatikana kupitia tovuti ya http://www.nactvet.go.tz:
- Mfumo wa Kuhakiki Udahili wa Wanafunzi (Student Information Verification)
- Mfumo wa Kuomba Namba ya Utambuzi wa Tuzo (AVN)
- Mfumo wa Kuomba Hati ya Matokeo (Transcript)
Mifumo hii inalenga kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanafunzi bila kulazimika kufika ofisi za NACTVET, hivyo kuongeza ufanisi na kuokoa muda.
Ushirikiano na TAHLISO
NACTVET itashirikiana kwa karibu na viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu nchini (TAHLISO) ili kuhakikisha elimu kuhusu matumizi ya mifumo hiyo inawafikia wanafunzi wengi zaidi.
Kupitia ushirikiano huu, elimu itatolewa moja kwa moja kwenye vyuo mbalimbali pamoja na kusambaza maudhui ya kidigitali kupitia mitandao ya kijamii, kwa lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi kujihudumia kidigitali.
Ziara Vyuo Mbalimbali
Kama sehemu ya kampeni, NACTVET pia itafanya ziara kwenye vyuo mbalimbali, ambako itatoa elimu ya moja kwa moja kwa wanafunzi na kuwaelekeza namna bora ya kutumia mifumo hiyo.
Soma zaidi:
Leave a comment