Toleo la FIFA Club World Cup 2025 litakuwa la kihistoria kwani ni mara ya kwanza kabisa mashindano haya yatashirikisha vilabu 32 kutoka mabara yote. Mashindano haya makubwa ya vilabu yatafanyika nchini Marekani kuanzia tarehe 15 Juni 2025, yakiwakutanisha mabingwa kutoka kila kona ya dunia. Afrika imepata nafasi nne (4) kwa klabu zilizofanya vizuri kwenye mashindano ya CAF Champions League kuanzia mwaka 2021 hadi 2024, hatua ambayo inaonyesha ukuaji na ushindani wa soka la Afrika.

Azam TV Kuwaletea Michuano Hii Moja kwa Moja
Kuelekea michuano hii mikubwa, kampuni ya Azam TV, inayojulikana kwa kurusha mechi kutoka ligi mbalimbali ndani na nje ya Afrika, imethibitisha kuwa itarusha moja kwa moja matangazo ya michuano yote ya FIFA Club World Cup 2025. Kupitia ukurasa wao wa Instagram, Azam TV imethibitisha kuwa mashabiki wa soka Tanzania na Afrika kwa ujumla watapata fursa ya kufurahia burudani hii ya aina yake, kuanzia mechi ya kwanza hadi fainali.
Channel Zitakazorusha Michuano:
Matangazo ya moja kwa moja yatapatikana kupitia chaneli zifuatazo za Azam TV:
- Azam Sports 3 HD
- Azam Sports 4 HD
Azam TV pia imewakumbusha wateja wake kuhakikisha wanahuisha (renew) kifurushi chao cha kisimbuzi mapema ili wasikose hata dakika moja ya burudani ya michuano hii ya kipekee inayokusanya wakali kutoka vilabu vikubwa duniani.
FIFA Club World Cup Live Ndani ya Azam TV – Kuanzia 15 Juni 2025!
Tazama historia ikiandikwa, ukiwa nyumbani kwako.