NECTA Matokeo ya Darasa la Nne 2023-24

NECTA Matokeo ya Darasa la Nne 2023-24

  • Posted by:
  • Posted on:
  • Category:
    ElimuElimu
  • System:
    Unknown
  • Price:
    USD 0

Leo katika makala360, Haya hapa Matokeo ya Darasa la Nne 2023-24 NECTA Katika Mkutano wake wa 157 uliofanyika tarehe 07 Januari, 2023 katika ofisi za Baraza la Mitihani la Tanzania zilizopo Dar es Salaam, Baraza la Mitihani la Tanzania liliidhinisha kutangazwa rasmi kwa matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne iliyofanyika mwezi Oktoba/Novemba, 2023.

Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne

Jumla ya wanafunzi 1,693,444 walisajiliwa kufanya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne wakiwemo Wasichana 864,482 sawa na asilimia 51.05 na Wavulana 828,962 sawa na asilimia 48.95.

Kati ya wanafunzi waliosajiliwa, wanafunzi 1,545,607 walifanya Upimaji, wakiwemo Wasichana 803,647 (92.96%) na Wavulana 741,960 (89.50%). Wanafunzi 147,837 (8.73%) hawakufanya Upimaji, kati yao Wasichana ni 60,835 (7.04%) na Wavulana ni 87,002 (10.50%).

Ufaulu wa Ujumla

Jumla ya wanafunzi 1,287,934 kati ya 1,545,330 wenye matokeo sawa na asilimia 83.34 wamefaulu kwa kupata Madaraja ya A, B, C na D. Mwaka 2022 Wanafunzi waliofaulu walikuwa 1,320,700 sawa na asilimia 82.95. Hivyo, kumekuwa na ongezeko la ufaulu kwa 2 asilimia 0.39 kwa wanafunzi waliopata fursa ya kuendelea na Darasa la Tano ikilinganishwa na mwaka 2022.

Idadi ya shule katika makundi ya Umahiri inaonesha kuwa, kati ya shule zote 19,264 zenye matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne 2023, shule 18,939 sawa na asilimia 98.31 zimepata wastani wa Daraja la A-D ikilinganishwa na shule 18,319 sawa na asilimia 98.27 zilizopata wastani wa madaraja hayo mwaka 2022. Hivyo, kumekuwa na ongezeko la asilimia 0.04 ya shule zilizopata wastani wa Daraja la A-D ikilinganishwa na mwaka 2022.

Angalia matokeo hapa.

Soma zaidi:

  1. Walioitwa Kwenye Usaili Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) 2025
Rating

0

( 0 Votes )
Please Rate!
NECTA Matokeo ya Darasa la Nne 2023-24

No votes so far! Be the first to rate this post.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *