
Ajira Portal login Page – Sekretarieti ya Ajira 2025 News Update Public Service Recruitment Secretariat kutuma maombi kujisajili kufungua akaunti kweka vyeti kuedit nakala huduma kwa wateja msaada pamoja na matangazo ya nafasi za kazi kutoka Taasisi mbalimbali utumishi.
Ajira Portal login Page
SEHEMU | MAELEZO MUHIMU |
---|---|
1. Taarifa Binafsi (Personal Details) | – Ingiza Namba ya NIDA- Mfumo utathibitisha kwa kukuuliza maswali mafupi- Taarifa kutoka NIDA zitajazwa moja kwa moja- Malizia taarifa nyingine kisha bonyeza Save |
2. Mawasiliano (Contact Details) | – Jaza: Sanduku la Posta, Barua Pepe, Anuani ya Makazi- Chagua: Nchi, Mkoa, Wilaya- Ingiza mwenyewe: Namba ya Simu |
3. Taarifa za Kitaaluma (Academic Qualifications) | – Chagua ngazi ya elimu (anzia kidato cha nne)- Chagua nchi uliyosoma- Chagua fani/programu sahihi kama ilivyo kwenye cheti- Andika jina kamili la chuo, si kifupi- Onyesha tarehe ya kuanza na kuhitimu– Ambatisha cheti kilichothibitishwa (kisiwe zaidi ya 2MB)- Bonyeza Save kuhifadhi taarifa |
Vidokezo Muhimu vya Elimu | – Ingiza cheti kimoja kimoja (PDF)– Tumia index number sahihi ya kidato cha nne/sita- Waliosoma nje: Ambatisha barua ya NECTA/NACTVET/TCU kulingana na ngazi ya elimu |
4. Kupoteza Cheti (CSEE/ACSEE) | – Bofya “Click here if you lost your certificate”– Ingiza index number na mwaka uliohitimu- Mfumo utatoa taarifa zako kutoka NECTA- Thibitisha na save kama taarifa ni sahihi |
5. Sehemu ya Maombi ya Kazi (My Application) | – Angalia hatua za maombi yako- Jua kama maombi yamepokelewa au la– Jua kama uko kwenye shortlist au sababu ya kutokuchaguliwa- Angalia kama umeitwa usaili na aina ya usaili (mahojiano, maandishi n.k.)- Jua kituo cha kazi ulichopangiwa |
6. Kuhariri Barua ya Maombi | – Unaweza kuhariri barua kama tangazo bado halijaisha muda- Bonyeza Edit, ambatisha barua mpya- Bonyeza Update ili kuhifadhi barua mpya |
Pakua hapa Mwongozo wa Mabadiliko Katika Matumizi ya Mfumo wa Maombi ya Kazi Kujisajili katika mfumo gusa hapa. Pia, Kuingia katika mfumo bonyeza hapa nafasi za kazi mbalimbali zilizotangazwa Utumishi angalia hapa.
Kama una swali uliza sasa.
Jinsi ya Kujiandaa kwa Ajili ya Usaili
1. Fika kwa Wakati (Utimamu wa Muda)
Hakikisha unafika mapema kwenye eneo la usaili. Inashauriwa kufika angalau nusu saa kabla ya muda rasmi. Tembelea eneo hilo mapema kabla ya siku ya usaili ili ujue mahali halisi ulipoitwa, muda wa kufika na mazingira ya pale. Hii itakupa nafasi zaidi ya kujiandaa kwa utulivu kabla ya usaili kuanza.
2. Vyeti Halisi vya Elimu ni Muhimu
Waombaji wote wanapaswa kufika kwenye usaili wakiwa na vyeti vyao halisi vya elimu. Mfano: Cheti cha Uzamivu (PhD), Uzamili (Masters), Shahada (Degree), Stashahada ya Juu (Advanced Diploma), Stashahada (Diploma), Cheti (Certificate), Kidato cha Sita (ACSEE), Kidato cha Nne (CSEE), na vyeti vingine kutoka katika taasisi za kitaaluma.
3. Tulia na Uwe Mtulivu
Wakati wa usaili, jaribu kuwa mtulivu na usipate wasiwasi. Chukua muda kidogo wa kutafakari kabla ya kujibu maswali. Hakikisha unadumisha mawasiliano ya macho (eye contact) na muhoji. Sikiliza swali lote kabla ya kujibu, na uwe makini – hutapenda kuonekana kama umesahau swali!
4. Onyesha Ujuzi na Maarifa Yako
Jaribu kuhusisha majibu yako na taarifa unazozijua kuhusu taasisi au kampuni unayoomba kazi. Unapozungumzia mafanikio yako, yaambatanishe na mahitaji ya nafasi ya kazi husika. Eleza kwa namna unavyolingana na mahitaji ya waajiri.
5. Fanya Utafiti
Ukikosa mpango, unajitayarisha kushindwa. Utaulizwa maswali maalum kuhusu taasisi husika, hivyo hakikisha umefanya utafiti wa kutosha kuhusu taasisi hiyo – mfano, mafanikio yao ya hivi karibuni, bidhaa walizozindua au miradi waliyoanzisha. Pia fahamu mwelekeo wa sekta husika kwa ujumla.
6. Fanya Mazoezi ya Kujibu Maswali
Ingawa kila usaili huwa tofauti, kuna maswali ya msingi ambayo karibu kila usaili huuliza. Jiandae kujibu maswali yanayohusu nguvu na udhaifu wako, historia yako ya kitaaluma na elimu, na pia eleza kwa nini wewe unastahili nafasi hiyo kuliko waombaji wengine.
7. Epuka Makosa Wakati wa Usaili
Usifanye makosa ya kawaida ambayo waombaji wengi hujikuta wakiyafanya. Jifunze makosa hayo mapema kabla ya kwenda kwenye usaili ili upunguze msongo wa mawazo baada ya usaili.
8. Fanya Mazoezi ya Usaili
Chukua muda kujifunza na kupitia maswali ya kawaida yanayoulizwa kwenye usaili. Hii itakusaidia kuwa na mfumo wa majibu na kupunguza hofu. Fanya mazoezi na rafiki au mwanafamilia. Ukifanya hivi, siku ya usaili halisi utakuwa na kujiamini zaidi.
9. Jiandae kwa Usaili wa Simu
Unapokuwa kwenye mchakato wa kutafuta kazi, kuwa tayari kwa usaili wa ghafla kupitia simu. Unaweza kupigiwa simu na mwajiri au mshauri na kuombwa kuzungumza. Jiandae mapema kwa kujua mbinu bora za kujibu maswali kwa simu bila kuchelewa au kuchanganyikiwa.
10. Mavazi ya Usaili
Vaa kwa heshima na staha kwa kuzingatia mazingira ya usaili. Mavazi yako yana mchango mkubwa katika mtazamo wa awali wa muajiri kwako. Muonekano wako wa kwanza una athari kubwa – ndivyo waajiri wanavyotoa taswira ya awali ya utu wako. Hivyo, ni muhimu kuvaa mavazi rasmi yanayoendana na nafasi ya kazi unayoomba.