Ili kuanza mchakato wa kujisajili na Ajira Portal, tembelea tovuti rasmi kupitia portal.ajira.go.tz. Kisha bofya sehemu iliyoandikwa Register au Jisajili. Utatakiwa kujaza taarifa zako binafsi kama vile jina kamili, tarehe ya kuzaliwa, jinsia, namba ya simu, barua pepe, na namba ya kitambulisho (NIDA). Hakikisha taarifa zote ni sahihi kabla ya kuendelea.

Ajira Portal ni tovuti rasmi ya serikali kupitia Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, inayorahisisha upatikanaji wa ajira serikalini. Kujisajili kwenye mfumo huu ni hatua muhimu kwa mtu yeyote anayetafuta kazi katika taasisi za serikali. Kupitia akaunti yako, utaweza kuwasilisha maombi ya kazi, kufuatilia mchakato wa maombi, na kupokea taarifa muhimu kuhusu ajira mpya.
Hatua za Kujisajili Ajira Portal:
- Tembelea tovuti rasmi https://portal.ajira.go.tz
- Bonyeza kitufe cha “Register” kwa ajili ya kujisajili kama mtumiaji mpya.
- Jaza taarifa zako binafsi kama vile majina kamili, namba ya kitambulisho (NIDA), barua pepe na namba ya simu.
- Unda nenosiri (password) utakayokumbuka kwa urahisi na kisha thibitisha usajili kupitia barua pepe.
- Baada ya kuthibitisha, ingia kwa kutumia email na password ulizochagua.
- Jaza Profile yako kwa ukamilifu (wasifu binafsi, elimu, uzoefu wa kazi, ujuzi, na viambatisho muhimu).
- Hifadhi mabadiliko na uanze kuomba kazi zilizotangazwa.
Vitu Muhimu vya Kuandaa Kabla ya Kujisajili Ajira Portal:
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya NIDA.
- Barua pepe inayofanya kazi.
- Namba ya simu inayopatikana muda wote.
- Vyeti vya elimu (cheti cha darasa la saba, kidato cha nne/sita, diploma/degree nk).
- Vyeti vya taaluma na kitaaluma (kama zipo).
- CV (Curriculum Vitae) iliyoandikwa vizuri.
- Picha ndogo ya pasipoti.
- Leseni ya kazi (kwa taaluma zinazohitaji kama udaktari, uhasibu nk).
Kwa kujisajili Ajira Portal, utaweza kushiriki kikamilifu katika mchakato wa ajira serikalini kwa uwazi na kwa njia ya kidigitali.
Sijaelewa hapo kwenye barua pepe inayofanya kazi
Soma mwongozo kwanza. Download hapo
Sorry mi nmejaza taarifa zote imefika 90% ila inagoma kutuma maombi shida itakuwa nini?
Wewe jaza kila kitu angalia program category uliyoisave. Kisha angalia kipengele baada ya kipengele huenda kuna sehemu umeparuka
Kwa mfano ulishajisajili na ukasahau email inakuaje apo wakuu
Naitaji msaada nilijisajili ajira portal kwenye email nyingine ile email niliyojisajiri imenipotea sasa nilijisajiri hii email ya sasa nikingiza taarifa zangu kwenye Nida inaniambia namba ya nida tayar ishatumika sijui nawezaje Tena kujisajili
Tembelea ofisi za Utumishi zilizopo DAR ES SALAAM (Posta) au DODOMA
Mimi nimejisajili ila ina niambia namba ya nida ninayoiambatanisha tayari Ipo kwenye portal ya health nafanyaje ili niweze kuifuta kwenye hiyo portal maana nili ji register kwamakosa kwenye hiyo portal
Portal ya health?