Please briefly explain why you feel this question should be reported.

Please briefly explain why you feel this answer should be reported.

Please briefly explain why you feel this user should be reported.

Makala 360

Makala 360

Makala 360 Navigation

Search
Ask A Question

Mobile menu

Close
Ask A Question
You can use WP menu builder to build menus
Home/ Questions/Q 1028

Makala 360 Latest Questions

Memo
  • 0
  • 0
MemoTeacher
Asked: June 17, 20252025-06-17T19:09:37+03:00 2025-06-17T19:09:37+03:00

Jinsi ya Kuomba AVN NACTVET

  • 0
  • 0
Jinsi ya Kuomba AVN NACTVET

Jinsi ya Kuomba AVN NACTVET Award Verification Number (AVN) Haya ni maelezo kuhusu uthibitisho wa vyeti na utaratibu wa kujiunga kwa wanafunzi waliomaliza stashahada kutoka vyuo vinavyotambuliwa na NACTE au TCU

Uthibitisho wa Cheti (Award Verification Number – AVN)

Ili kupata namba ya uthibitisho wa cheti (AVN), mwanafunzi lazima awe amehitimu Stashahada (Diploma) kutoka chuo kinachotambulika na:

  • NACTE (Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi) au
  • TCU (Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania)

Masharti na Utaratibu wa Kuomba

Kwa wanafunzi waliomaliza Stashahada

  1. Mwaka 1961 hadi 2014:
    • Wapakie cheti cha Diploma pamoja na nakala ya matokeo (Transcript) kwa mfumo wa PDF.
  2. Walio na Cheti cha Ufundi Kamili (FTC) kutoka NECTA:
    • Wanaweza kutumia namba yao ya mwisho ya mtihani kama ilivyo kwenye cheti. Mfano: U0000/0000/0000.
  3. Waliomaliza kuanzia 2015 hadi sasa:
    • Lazima wawe na matokeo yanayotambulika na chuo na yaliyopo kwenye mfumo wa NACTE.
    • Format ya namba inaweza kuwa:
      • NSXXXX/XXXX/XXXX
      • NPXXX/XXXX/XXXX
      • Au nyingine yoyote iliyosajiliwa chuoni (Wasiliana na Afisa wa Udahili wa chuo husika).

Vigezo vya Elimu ya Sekondari

  1. Wote wanatakiwa kuwa na Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE)
    • Na angalau pass nne (4) katika masomo yasiyo ya kidini.
  2. Waliomaliza CSEE kabla ya 1988, au Walimu kabla ya 2010, au wenye vyeti vya kabla ya 2015:
    • Wapakie vyeti na transcript zao za masomo.

Wenye Vyeti vya Kigeni

  1. Wenye elimu ya sekondari kutoka nje ya Tanzania:
    • Lazima waombe usawa wa vyeti kutoka NECTA.
  2. Wenye stashahada kutoka nje ya nchi:
    • Wapate usawa wa vyeti kutoka NACTE.

Jinsi ya Kuhakiki Taarifa za Mwanafunzi kwa Ajili ya AVN

HatuaMaelezo
1Tembelea tovuti ya NACTE https://www.nactvet.go.tz
2Bofya “Students Information Verification”
3Weka namba ya mtihani wa CSEE au namba ya usajili wa Diploma
4Kama umesahau nenosiri (password), bofya “Forgot Password”
5Ingiza jina la mtumiaji, namba ya simu au barua pepe uliyotumia kusajili
6Mfumo utatuma nenosiri jipya kwenye namba ya simu na barua pepe yako

Kwa Wahitimu Kutoka Vyuo Hivi

Wanafunzi waliomaliza kutoka vyuo vifuatavyo wanapaswa kuhakikisha taarifa zao zipo kwenye mfumo wa NACTE:

  • Dar es Salaam Institute of Technology (DIT)
  • Mbeya University of Science and Technology (MUST)
  • Arusha Technical College (ATC)
  • Karume Institute of Science and Technology (KIST)
  • 0 0 Answers
  • 0 Followers
  • 0
  • Share
    Share
    • Share on Facebook
    • Share on Twitter
    • Share on LinkedIn
    • Share on WhatsApp
Leave an answer

Leave an answer
Cancel reply

Sidebar

Trending

Ajira DEREVA HESLB Kazini MASASI MDAs & LGAs Mshahara SIKONGE Usaili Utumishi

Explore

© 2025 Makala 360. All Rights Reserved
Created by Makala360