Majina ya waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi kwa mwaka 2025 tayari yametangazwa. Waombaji waliofanikiwa wametakiwa kuripoti katika vituo maalum vilivyopangwa kwa ajili ya kuanza mafunzo ya kijeshi.

Kwa vijana waliofanyiwa usaili katika maeneo ya Dar es Salaam na vikosi vya Makao Makuu ya Polisi, wametakiwa kuripoti katika eneo la Polisi Baracks, Barabara ya Kilwa, karibu na Hospitali ya Polisi, kuanzia tarehe 30 Septemba 2024 saa 12:00 asubuhi, kwa ajili ya maandalizi ya safari kuelekea Shule ya Polisi Moshi.
- Angalia majina hapa https://polisi.go.tz/ajira
Wale waliofanya usaili katika mikoa mingine ya Tanzania Bara wanapaswa kuripoti kwa makamanda wa polisi wa mikoa yao mnamo tarehe 29 Septemba 2024 saa 2:00 asubuhi, ambapo watapewa maelekezo ya safari kuelekea Moshi.
Mafunzo hayo ni sehemu ya mchakato wa kuwaandaa vijana kwa ajili ya kujiunga rasmi na Jeshi la Polisi, baada ya kukamilisha hatua zote za mafunzo na tathmini.