Hii hapa orodha ya Majina ya Waliochaguliwa JKT 2025 (Jeshi la Kujenga Taifa JKT) Wito wa Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria kwa Wahitimu wa Kidato cha Sita Mwaka 2025 Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, anatoa wito kwa vijana wote wa Tanzania Bara waliomaliza elimu ya sekondari kidato cha sita mwaka 2025, kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria yatakayoanza rasmi mwaka huo.

Kwa mujibu wa JKT, vijana hao wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 28 Mei hadi 08 Juni 2025 kwa ajili ya mafunzo hayo muhimu ya kujenga uzalendo na ustadi wa maisha.
- Angalia hapa orodha ya majina ya waliochaguliwa JKT 2025 PDF
- Tangazo la wito kwa kidato cha sita waliochaguliwa kujiunga JKT
Makambi ya JKT Waliyopangiwa Wahitimu
Vijana wamepangwa katika kambi mbalimbali nchini kama ifuatavyo:
- Mara: JKT Rwamkoma
- Tabora: JKT Msange
- Pwani: JKT Ruvu, JKT Kibiti
- Dodoma: JKT Makutupora
- Iringa: JKT Mafinga
- Ruvuma: JKT Mlale
- Tanga: JKT Mgambo, JKT Maramba
- Arusha: JKT Makuyuni, JKT Orjolo
- Kigoma: JKT Bulombora, JKT Kanembwa, JKT Mtabila
- Songwe: JKT Itaka
- Rukwa: JKT Luwa, JKT Milundikwa
- Lindi: JKT Nachingwea
- Pwani (Mlandizi): Kwa wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho – JKT Ruvu
Vifaa Muhimu vya Kujiandaa Navyo Kabla ya Kuripoti
Wahitimu wote wanatakiwa kuripoti makambini wakiwa na vifaa vifuatavyo:
- Bukta ya rangi ya bluu iliyokolea (Dark Blue) yenye mpira kiunoni na mfuko mmoja nyuma.
- T-shirt ya rangi ya kijani.
- Raba za michezo za rangi kijani au bluu.
- Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
- Soksi ndefu za rangi nyeusi.
- Nguo za kuhifadhi joto kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
- Track suit ya rangi ya kijani au bluu.
- Nyaraka zote muhimu za udahili kama cheti cha kuzaliwa, vyeti vya kidato cha nne na sita, n.k.
- Nauli ya kwenda na kurudi kutoka kambini.
Namna ya Kupata Orodha ya Majina na Kambi
- Tembelea tovuti rasmi ya JKT kupitia: http://www.jkt.mil.tz
- Ingiza jina la shule au namba ya shule ya sekondari ya kidato cha sita.
- Bonyeza neno “Waliochaguliwa” ili kuona jina lako, kambi, mkoa na wilaya ulipopangiwa.
- Kupakua orodha kamili ya majina na taarifa nyingine, pakua faili la “JKT PDF 2025” lililopo juu kulia kwenye ukurasa huo.
Mwito kwa Vijana wa Kitanzania
Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Mabele, anawakaribisha kwa moyo mkunjufu vijana wote waliomaliza kidato cha sita mwaka 2025 kujiunga na mafunzo haya. Kupitia JKT, vijana watapata:
- Mafunzo ya uzalendo
- Kujenga umoja wa kitaifa
- Kupata stadi za kazi na maisha
- Kukuza utayari wa kulitumikia Taifa
Tembelea sasa: http://www.jkt.mil.tz
Tarehe ya kuripoti: 28 Mei – 08 Juni 2025
TZ JKT – Kulea Uzalendo, Kukuza Taifa!