TRA Yatangaza Matokeo ya Usaili wa Mahojiano – Jumla ya Ajira 1,896 Kupatikana (Oral Interview) Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inakumbusha umma kwamba mnamo Februari 2025, ilitangaza nafasi za ajira zipatazo 1,596, ambapo ilipokea jumla ya maombi 135,027 kutoka kwa Watanzania waliovutiwa. Baada ya mchujo wa awali, waombaji 113,023 walikidhi vigezo na kualikwa kwenye usaili wa kuandika uliofanyika tarehe 29 na 30 Machi, 2025.

Wasailiwa waliofaulu usaili wa maandishi waliendelea kwenye usaili wa mahojiano uliofanyika kati ya tarehe 12 hadi 14 Mei, 2025, ambapo 6,325 walishiriki.
Kwa kutambua hitaji kubwa la ajira, Mamlaka inapenda kutoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuridhia kuongeza nafasi za ajira 300 zilizokuwepo kwenye Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2026. Hii imeongeza jumla ya nafasi za ajira kutoka 1,596 hadi 1,896.
Taarifa Muhimu kwa Washiriki wa Usaili
TRA inawatangazia waombaji wote waliopitia usaili wa mahojiano kwamba matokeo rasmi ya usaili huo yatatolewa kesho, tarehe 28 Mei 2025, kupitia barua pepe walizotumia kuwasilisha maombi ya kazi.
Waombaji 1,896 waliopata ajira wanapaswa kufika katika kumbi walizopangiwa tarehe 02 Juni, 2025 saa 1:00 asubuhi wakiwa na nyaraka zote muhimu kama ilivyoelekezwa kwenye barua pepe.
Fursa kwa Wasiofanikiwa
TRA inatambua juhudi za waombaji wote na kwa namna ya kipekee, inawapongeza waombaji 4,429 ambao walishiriki usaili wa mahojiano lakini hawakupata nafasi. Taarifa zao zimehifadhiwa katika kanzidata ya Mamlaka kwa ajili ya fursa za ajira zijazo.
Mawasiliano
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na TRA kupitia:
- Tovuti: http://www.tra.go.tz
- Simu Bila Malipo: 0800 780078 | 0800 750075 | 0800 110016
- WhatsApp: 0744 23 33 33
- Barua Pepe: huduma@tra.go.tz | services@tra.go.tz
Soma zaidi:-