Nafasi za Kazi TASHICO, TMA – Ajira 59 Kwa niaba ya Tanzania Shipping Company Limited (TASHICO) na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inakaribisha Watanzania wote wenye sifa na wanaopenda kufanya kazi, kuomba nafasi 59 za kazi zilizopo, kama zilivyoelezwa.

Vitu Muhimu vya Kuzingatia kwa Waombaji wa Ajira
Ikiwa unapanga kutuma maombi ya ajira kupitia Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, hakikisha unazingatia masharti na maelekezo yafuatayo:
Sifa za Jumla
- Lazima uwe raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45.
- Watu wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na waeleze waziwazi kwenye mfumo wa maombi ili kupewa kipaumbele.
- Wafanyakazi wa serikali hawaruhusiwi kuomba kwa mujibu wa Waraka wa Ajira Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Wastaafu wa utumishi wa umma kwa sababu yoyote hawaruhusiwi kuomba.
Nyaraka Muhimu za Kuambatanisha
Waombaji wanapaswa kuambatanisha nakala zilizothibitishwa za vyeti vifuatavyo:
- Cheti cha Uzamili, Shahada, Diploma ya Juu, Diploma au Cheti
- Transcript za Uzamili, Shahada, Diploma ya Juu au Diploma
- Vyeti vya kidato cha nne na sita
- Vyeti vya usajili wa kitaaluma au mafunzo maalum (ikiwa inahitajika)
- Cheti cha kuzaliwa
- Picha ya pasipoti ya hivi karibuni
Vyeti Visivyokubalika
HAIRUHUSIWI kuambatanisha vyeti vifuatavyo:
- “Results slip” za kidato cha nne au sita
- “Testimonial” au “Partial transcripts”
Taarifa Binafsi na Wasifu
- Ambatanisha CV ya kisasa yenye taarifa kamili na sahihi za mawasiliano: anuani, sanduku la posta, barua pepe na namba ya simu.
- Taja watu watatu wa rufaa (reputable referees) na mawasiliano yao kamili.
Vyeti vya Elimu kutoka Nje ya Nchi
- Vyeti vya kidato cha nne na sita kutoka nje lazima vithibitishwe na NECTA.
- Vyeti vya taaluma kutoka vyuo vya nje lazima vithibitishwe na TCU (kwa elimu ya juu) au NACTE (kwa vyuo vya ufundi).
Uwasilishaji wa Maombi
- Barua ya maombi lazima iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza, ikusainiwe, na ipelekwe kwa anuani ifuatayo:
Katibu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
S.L.P 2320,
Jengo la Utumishi,
Chuo Kikuu cha Dodoma – Majengo ya Dr. Asha Rose Migiro,
Dodoma.
- Maombi yatumwe kupitia mfumo wa kielektroniki kupitia tovuti http://portal.ajira.go.tz/
(Tovuti hii pia inapatikana kupitia tovuti ya PSRS, bonyeza ‘Recruitment Portal’)
Tarehe Muhimu
- Mwisho wa kutuma maombi: 08 Juni, 2025
- Ni waombaji waliopitia mchujo pekee watakaojulishwa kuhusu tarehe ya usaili.
Onyo Muhimu
- Uwasilishaji wa vyeti vya kughushi au taarifa za uongo utasababisha hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi ya mhusika.
Soma zaidi:-