
Nafasi za Kujiunga na Vyuo baada ya matokeo kwa Wanafunzi wa Kidato cha Sita 2025
Aina ya Chuo/Taasisi | Sifa Muhimu za Kujiunga | Kozi Zinazotolewa | Muda wa Masomo | Maelezo ya Ziada |
---|---|---|---|---|
Vyuo Vikuu (Universities) | Angalau Principal Passes mbili (D au zaidi) katika masomo ya combination | Shahada (Bachelor Degree) | Miaka 3 – 5 | TCU hupanga udahili kupitia CAS (Central Admission System) |
Vyuo Vikuu Vishiriki | Kama vyuo vikuu vikuu – D+ mbili au zaidi | Bachelor na Diploma | Miaka 3 – 4 | Mara nyingi huendesha kozi maalum kama elimu, biashara, n.k. |
Vyuo vya Ufundi (Technical) | D mbili au C katika masomo ya sayansi/technolojia | Engineering, ICT, Architecture, Electronics | Miaka 2 – 4 | NACTVET husimamia usajili wa vyuo hivi |
Vyuo vya Ualimu | D mbili au zaidi kwa masomo ya kufundishia (Maths, English, Kiswahili, n.k.) | Diploma ya Ualimu, Bachelor of Education | Miaka 2 – 3 | Udahili hupangwa na TAMISEMI au vyuo vyenyewe |
Vyuo vya Afya | Biology, Chemistry, Physics angalau D kila moja | Clinical Medicine, Nursing, Pharmacy | Miaka 2 – 4 | Vigezo huwa vikali zaidi, hasa kwa kozi ya Udaktari |
Vyuo vya Biashara | D mbili au zaidi katika masomo ya biashara (e.g. Econs, Commerce, Accounts) | Diploma na Degree za Business, Procurement, ICT | Miaka 2 – 4 | Mifano: CBE, IFM, TIA, NBMM |
Vyuo vya Kati (Middle Level) | Kuanzia E hadi D katika masomo yanayohusiana na kozi | Diploma, Certificate | Miaka 1 – 2 | Hupokea waliofeli kidogo, lakini bado wana sifa za kozi ya kati |
Vyuo vya Kijeshi/Vya Polisi | D mbili au zaidi; nidhamu, afya njema, na mahojiano ya kina | Mafunzo ya kijeshi, Polisi, Jeshi la Magereza | Tofauti kulingana na taasisi | Masharti ya usaili huwa ya kimwili, kitaaluma, na kiusalama |
Mambo Muhimu Kufanya Baada ya Matokeo
- Tembelea tovuti ya TCU au NACTVET ili kuanza udahili (TCU: kwa vyuo vikuu, NACTVET: kwa diploma/certificate).
- Chagua kozi kwa uangalifu kulingana na alama zako na matakwa ya ajira au ujuzi.
- Tafuta mikopo ya elimu ya juu (HESLB) kama unahitaji msaada wa ada na gharama nyingine.
- Jiandae na nyaraka muhimu kama cheti cha kuzaliwa, vyeti vya matokeo, picha za pasipoti, nk.