
NECTA Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 (ACSEE)- 2025/2026 PDF ni matokeo form six ya mwisho kwa wanafunzi wa elimu ya sekondari ya juu nchini Tanzania waliomaliza kidato cha sita. Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) linayatarajiwa kutangaza matokeo hayo kati ya mwisho wa Julai hadi wiki ya kwanza ya Agosti 2025.
Wanafunzi wataweza kuyapata kupitia tovuti rasmi ya NECTA au kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu (SMS/USSD). Matokeo haya ni muhimu kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na elimu ya juu, kwani ufaulu wao utaamua sifa za kuingia vyuo vikuu au taasisi nyingine za elimu ya juu kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026.
Matokeo ya Kidato cha Sita 2025
Kipengele | Maelezo |
---|---|
Jina la Mtihani | Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) 2025 |
Mamlaka Inayohusika | Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) |
Wanafunzi Waliopaswa Kufanya | Wanafunzi wote wa Kidato cha Sita Tanzania Bara na Zanzibar waliohitimu 2025 |
Tarehe za Mtihani | Mei – Juni 2025 |
Tarehe ya Kutangazwa Matokeo | Inatarajiwa mwishoni mwa Julai hadi wiki ya kwanza ya Agosti 2025 |
Njia za Kupata Matokeo | 1. Tovuti ya NECTA (https://www.necta.go.tz)2. Kwa SMS/USSD: *152*00# → Elimu → NECTA |
Alama za Ufaulu | A (Bora Zaidi), B+, B, C, D, E, F (A ni ya juu, F ni kufeli) |
Vigezo vya Kujiunga na Vyuo | Alama angalau D+ katika masomo mawili ya kombinesheni |
Faida za Matokeo | Kupata nafasi za udahili katika vyuo vikuu, vyuo vya kati, mafunzo ya kazi, au ajira ya kijeshi |
Tatizo la Matokeo | Wanafunzi wasioridhika wanaweza kukata rufaa kwa NECTA kwa kupitia shule au barua binafsi |
Wasiliana na NECTA | Simu: +255 22 277 5966 / Barua pepe: info@necta.go.tz |
Tovuti Rasmi | http://www.necta.go.tz |
Jinsi ya kuangalia Matokeo ya Form Six 2025
1. ACSEE 2025 Examination Results Enquiries Angalia hapa
2. NECTA Matokeo online Angalia hapa