Selection Form Five 2025 to 2026 Uchaguzi wa waliochaguliwa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano kwa mwaka wa masomo 2025/2026 unaratibiwa na TAMISEMI (Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa). Huu ni mchakato muhimu unaowapangia wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2024 na kufaulu mtihani wao (CSEE), kwenda katika shule za sekondari za Kidato cha Tano (A-Level) au vyuo vya ufundi na ufundi stadi, kulingana na ufaulu wao, mchepuo waliouchagua kupitia mfumo wa Selform, pamoja na nafasi zilizopo mashuleni au vyuoni.

Matokeo ya uchaguzi huu hutangazwa kwa kawaida kati ya mwezi Mei hadi Juni 2025 kupitia tovuti rasmi ya TAMISEMI: selform.tamisemi.go.tz. Wanafunzi wanaweza kuangalia shule au chuo walichopangiwa kwa kuchagua mkoa, wilaya, na shule waliyosoma, kisha kupakua “joining instructions” ambazo zinaeleza tarehe ya kuripoti, ada, na mahitaji mengine muhimu.
Mchakato huu huwa na awamu mbalimbali kama ya kwanza, pili na wakati mwingine ya tatu — hasa kwa ajili ya kujaza nafasi zilizobaki. Kipaumbele huwa kinatolewa kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi, ambao mara nyingi hupangiwa shule maarufu kama Ilboru, Mzumbe, na nyinginezo. Wengine hupangiwa shule za kitaifa za bweni au kutwa kulingana na sifa zao.
Wanafunzi ambao hawakupata nafasi kwenye uchaguzi wa kwanza wanaweza kuendelea kufuatilia tovuti ya TAMISEMI kwa ajili ya matokeo ya awamu zinazofuata. Pia, wanaweza kuangalia uwezekano wa kujiunga na shule binafsi au vyuo vya ufundi. Sifa za kujiunga na shule za serikali hutegemea alama za mchepuo aliochagua mwanafunzi, mfano PCB, HGL n.k.