Haya hapa majina ya walioitwa kazini Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 14-08-2024 na tarehe 05-04-2025 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo yameorodheshwa katika tangazo hili. Orodha hii pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Wasailiwa wote waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi watapaswa kupata barua zao za kupangiwa vituo vya kazi kupitia akaunti zao za Ajira Portal, sehemu ya My Applications. Baada ya kupakua barua hizo, wanapaswa kuzipakua (Download) na kuzichapisha (Print), kisha kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa kwa mujibu wa maelekezo yaliyomo kwenye barua husika angalia hapa majina.
Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi wanapaswa kuripoti kwa Mwajiri katika muda uliopangwa wakiwa na vyeti halisi vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na Mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira. Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili, watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili na hivyo wasisite kuomba tena nafasi za kazi zitakapotangazwa.
Kwa Muhtasari:
- Matokeo yameorodheshwa kwenye tangazo hili, wakiwemo waliofanikiwa kutoka kanzidata.
- Barua za kupangiwa vituo vya kazi zinapatikana kupitia Ajira Portal, sehemu ya My Applications.
- Waombaji waliofanikiwa wanapaswa kuripoti kwa Mwajiri wakiwa na vyeti halisi vya masomo kama ilivyoainishwa kwenye barua zao za kupangiwa kituo cha kazi.