Orodha ya majina ya Waliochaguliwa JKT 2025 (Kidato cha Sita JKT) PDF Angalia hapa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linawakaribisha vijana wote waliomaliza kidato cha sita mwaka 2025 kutoka Tanzania Bara kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria jkt.mil.tz.. Vijana wametakiwa kuripoti makambini kati ya tarehe 28 Mei hadi 08 Juni 2025 katika makambi waliopangiwa. Orodha kamili ya majina, kambi na maeneo husika inapatikana kupitia tovuti rasmi ya JKT.

Vijana wamegawanywa katika makambi mbalimbali ikiwemo Rwamkoma (Mara), Msange (Tabora), Ruvu na Kibiti (Pwani), Mafinga (Iringa), Makutupora (Dodoma), Nachingwea (Lindi), Mpwapwa (Dodoma), Luwa na Milundikwa (Rukwa), Itaka (Songwe), Mlale (Ruvuma), Mgambo na Maramba (Tanga), Makuyuni na Orjolo (Arusha), Bulombora, Kanembwa na Mtabila (Kigoma). Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho wanapaswa kuripoti katika Kambi ya Ruvu – Mlandizi, Pwani.
- Angalia hapa orodha ya majina ya waliochaguliwa JKT 2025 PDF
- Tangazo la wito kwa kidato cha sita waliochaguliwa kujiunga JKT
Kabla ya kuripoti, vijana wanatakiwa kujiandaa na vifaa vifuatavyo:
- Bukta ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni, mfuko mmoja nyuma, bila zipu
- T-shirt ya kijani
- Raba za michezo za kijani au blue
- Shuka mbili za blue bahari
- Soksi ndefu nyeusi
- Nguo za baridi kwa waliopangiwa mikoa ya baridi
- Track suit ya kijani au blue
- Nyaraka muhimu za udahili (cheti cha kuzaliwa, vyeti vya kidato cha nne na sita)
- Nauli ya kwenda na kurudi kambini