Walioitwa Kazini TRA 2025, Baada ya matokeo ya Usaili Kutangazwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inafuraha kuwataarifu waombaji wote kuhusu hatua zilizofikiwa katika mchakato wa ajira uliotangazwa mwezi Februari 2025, ambapo nafasi 1,596 za kazi zilitangazwa kwa umma.

Katika mchakato huo, TRA ilipokea maombi 135,027, na baada ya uchambuzi wa awali, waombaji 113,023 waliitwa kwenye usaili wa maandishi uliofanyika tarehe 29–30 Machi, 2025.
Baada ya hatua hiyo, waombaji waliopasi waliendelea kwenye usaili wa mahojiano uliofanyika kati ya tarehe 12 hadi 14 Mei, 2025, ambapo jumla ya 6,325 walishiriki.
Rais Aridhia Kuongezwa kwa Nafasi 300 za Ajira
Kwa heshima na shukrani za dhati, TRA inamshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuridhia ombi la kuongeza nafasi nyingine 300 za ajira. Hii imeifanya jumla ya nafasi zinazojazwa kupitia mchakato huu kufikia 1,896, badala ya zile 1,596 za awali.
Matokeo Kutolewa Rasmi Tarehe 28 Mei 2025
TRA inapenda kuwataarifu waombaji wote waliopitia hatua ya usaili wa mahojiano kwamba matokeo rasmi yatatolewa tarehe 28 Mei 2025 kupitia barua pepe walizotumia kuwasilisha maombi.
Waombaji 1,896 waliopata ajira wanatakiwa kufika kwenye vituo walivyopangiwa tarehe 02 Juni 2025 saa 1:00 asubuhi, wakiwa na nyaraka zote muhimu kama ilivyoelekezwa kwenye barua pepe zao.
Taarifa Zatahifadhiwa kwa Ajira Zijazo
Kwa waombaji 4,429 waliopata nafasi ya usaili wa mahojiano lakini hawakupata ajira, TRA inatoa shukrani za dhati kwa ushiriki wao. Taarifa zao zitahifadhiwa kwenye kanzidata ya Mamlaka kwa ajili ya kuzingatiwa katika fursa zijazo.
Mawasiliano ya TRA
Kwa maelezo zaidi au msaada, tafadhali wasiliana nasi kupitia:
- Tovuti: http://www.tra.go.tz
- Namba za simu bila malipo:
- 0800 780078
- 0800 750075
- 0800 110016
- WhatsApp: 0744 23 33 33
- Barua Pepe: huduma@tra.go.tz | services@tra.go.tz.
Soma zaidi:-