- Posted by:
- Posted on:
- Category:
AjiraAjira - System:
Unknown - Price:
USD 0
Leo katika makala360, Hii hapa orodha ya majina ya Walioitwa Kwenye Mafunzo Jeshi la Zimamoto 2025 Orodha ya Waliochaguliwa Kuhudhuria Mafunzo ya Uaskari – Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatangaza rasmi majina ya waombaji waliochaguliwa kuhudhuria mafunzo ya Uaskari ngazi ya Konstebo.
Tarehe ya Kuripoti Chuoni
Wote waliochaguliwa wanapaswa kuripoti katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji – Chogo, Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga, kuanzia:
- Tarehe: 16 Mei 2025 hadi 18 Mei 2025
- Muda wa Mapokezi: Saa 12:00 asubuhi hadi saa 4:00 usiku
Mtu yeyote atakayeshindwa kufika ndani ya muda uliopangwa hatapokelewa, na nafasi yake itapewa mtu mwingine.
Maelekezo ya Usafiri
- Shuka kituo cha Kabuku, ambacho kiko takribani kilomita 12 kutoka chuoni.
- Chuo kimeandaa utaratibu wa kuwapokea waalikwa wote kuanzia tarehe zilizotajwa.
Gharama na Mahitaji ya Msingi
Mhusika anapaswa kujigharamia:
- Nauli ya kwenda chuoni
- Chakula na malazi hadi atakapopokelewa rasmi
Nyaraka Muhimu za Kuleta
Kila mhusika anapaswa kuja na:
- Vyeti halisi vya masomo na taaluma
- Cheti cha kuzaliwa
- Kitambulisho cha NIDA au namba ya NIDA
- Leseni hai ya udereva (kwa walioomba nafasi ya udereva)
- Vyeti vyote viwe na nakala tatu (3) kwa kila kimoja.
- Jina liwe sawa kwenye vyeti vyote—tofauti yoyote itasababisha kurejeshwa na nafasi kuchukuliwa na mwingine.
Ukaguzi wa Afya
Mhusika atapimwa:
- Afya ya mwili
- Afya ya akili
- Kipimo cha mimba kwa wanawake
Yeyote atakayebainika kuwa na matatizo ya kiafya hataruhusiwa kuendelea na mafunzo.
Vifaa vya Kuleta Chuoni
Mafunzo haya yanahitaji ulete vifaa vifuatavyo:
- Mashuka 2 ya bluu
- Mto 1 na foronya 2 za bluu
- Chandarua cha duara rangi ya bluu
- Ndoo ya plastiki (lita 20)
- Sahani na kikombe cha bati
- Fedha kidogo kwa matumizi binafsi
- Bima ya afya (kwa waliyo nayo)
Vifaa vya kununua Chuoni
Vifaa vifuatavyo vitanunuliwa katika duka la chuo:
- Raba za michezo
- Fulana (T-shirt) ya rangi ya bluu
- Madaftari makubwa (Counter books 4 quire – pcs 5)
- Vifaa vya michezo (track suit, bukta ya bluu, fulana)
- Kalamu
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linawapongeza waliochaguliwa na linatarajia ushirikiano mzuri katika hatua ya awali ya kujiunga na mafunzo.
Soma makala zaidi: