Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatekeleza mradi wa miaka mitano (2021/2022- 2025/2026) wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (Higher Education for Economic Transformation (HEET)). Kupitia mradi wa HEET Wizara imetenga fedha kwa ajili ya ufadhili wa masomo katika Programu ya Msingi kwa wanafunzi wa kike waliopungukiwa na sifa kidogo za kujiunga na masomo ya elimu ya juu katika masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STUH). Programu hiyo itatolewa katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (CKHT).

Wanafunzi watakaohitimu na kufauli masomo katika programu hii kwa viwango vilivyowekwa watapata fursa ya kuomba udahili katika taasisi za Elimu ya juu nchini kwa kufuata taratibu zilizoainishwa na TCU, NACTIVET na chuo husika, ikiwa ni pamoja na sifa za kuomba mkopo wa masomo ya elimu ya juu kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania bara na Tanzania visiwani. Waombaji wanaotoka Mikoa ambayo kijiografia haijafaidika, walemavu, yatima, familia masikini na zinazohudumiwa na TASAF na asasi zinazotambulika watapewa kipaumbele. Maombi yaambatishe vielelezo vilivyotajwa kutoka kwa wenye mamalaka ya kutoa vielelezo hivyo kama Daktari, TASAF, RITA, serikali za mitaa pamoja na nyeti vya kuhitimu.
CKHT kinayo furaha kutangaza awamu ya kwanza kwa mwaka 2025/2026 ya nafasi za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kike wenye sifa zinazohitajika ili kujiunga na programu hii maalumu.
SIFA ZA KUJIUNGA
Muombaji ataweza kukubaliwa kujiunga kwenyě programu husika endapo atakuwa na vigezo vingine muhimu vifuatavyo:
- Cheti cha Mtihani wa Elimu ya Sekondari (Kidato cha NNE) kikiwa na ufaulu angalau kwenye masomo manne ambayo yamepatikana kabla ya kufanya mtihani wa juu wa
- Elimu ya sekondari au ufaulu unaofanania na chochote kati ya vifuatavyo:
- Cheti cha Juu cha Mtihani wa Elimu ya Sekondari (Kidato cha SITA) kwenye masomo ya sayansi(Fizikia, Kemia,Baolojia, Hisabati, Uchumi na Jiografia) na angalau alama 1.5 kutoka kwenye masomo MAWILI
- Diploma katika masomo ya STUH kutoka kwenye chuo kinachotambulika yenye ufaulu wa GPA ya 2.0 mpaka 2.9.
- NTA Level 5/Professional Technician Level II Certificate.
Mimi ni mwanafunzi wa diploma katika masomo ya teknolojia na nahitajii kujiunga na elimu ya degree kwa ufaulu unaozidi GPA 2.9 Je naweza kunufaika na mradi huu